content stringlengths 1k 24.2k | category stringclasses 6
values |
|---|---|
JESHI la Polisi Tanzania, Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), limewasilisha mifumo miwili ya teknolojia katika mkutano wa Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na limesema lipo tayari kuipeleka katika nchi zote za jumuiya hiyo zisizo na teknolojia hiyo. Mifumo hiyo iliyobuniwa... | kitaifa |
Na Malima Lubasha-Musoma MAHAKAMA Kuu Kanda ya Musoma, imewahukumu
kunyongwa hadi kufa watu watatu kwa kosa la kumuua Tabu Makanya (58) kwa
kumchinja na kutenganisha kichwa na kiwiliwili. Waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa ni Musiba
Maregeba, Abeid Casimil na Ndaro Sumuni wote wakazi Kijiji cha Kwibara Kata ya
Mugango W... | kitaifa |
NA MWAMVITA MTANDA-KIGALI KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amefichua kuwa alifanya jitihada za kumshawishi aliyekuwa mshambuliaji wa timu hiyo, Emmanuel Okwi ili asalie Msimbazi, lakini nyota huyo wa kimataifa wa Uganda aligoma katakata. Okwi mwenye umri wa miaka 27, ameachana na Simba, baada ya mkataba wake kum... | michezo |
WASHINGTON, MAREKANI WAGOMBEA urais wa chama cha Democrat nchini Marekani wamemlaumu Rais Donald Trump baada ya kutokea visa viwili vya mashambulizi ya bunduki vilivyosababisha vifo vya watu 29 Texas na Ohio. Wagombea hao wanasema matamshi ya Trump ya kibaguzi dhidi ya walio wachache nchini humo yanachochea mgawanyiko... | kimataifa |
Na NORA DAMIAN,
MWANAFUNZI Cynthia Mchechu, ambaye ameshika nafasi ya pili kitaifa kwenye matokeo ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika Novemba mwaka jana, amesema Rais Mstaafu wa Marekani, Barack Obama, amechangia mafanikio yake.
Cynthia aliyekuwa akisoma Shule ya Sekondari ya Wasichana ya St. Francis Mbe... | kitaifa |
Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF) limeandaa kongamano la kitaifa kujadili masuala ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa shirika hilo Koshuma Mtengeti amesema, lengo la kongamano hilo ni kutafuta namna ya kutokomeza ukatili kwenye jamii.Kongamano h... | kitaifa |
Msanii wa Bongo fleva Diamond Platinumz ameamua kufanyia kufuru msanii wake aliyemsajili hivi karibuni ‘Zuchu’. Zuchu ambaye ni mtoto wa msanii Hadija Koppa alisajiliwa na lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) Aprili 8. Tangu kusajiliwa mwamadada huyo katika lebo hiyo kubwa ya muziki nchini Nyota wa Bongo Fleva Diamondi a... | burudani |
MKUU wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti ameagiza kukamatwa mara moja kwa mawakala wawili wa kampuni binafsi wanaopita vijijini wilayani Karagwe na Kyerwa kwa tuhuma za kuwapotosha na kuwalaghai wakulima wa kahawa wasikubaliane na mfumo wa serikali.RC Gaguti alitoa maelekezo hayo katika mkutano wa viong... | kitaifa |
Na AGATHA CHARLES – Dar es Salaam
MBUNGE wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete, amesema hatamani kuwa rais bali anataka siku moja awe Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam jana alipohojiwa katika kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na Televisheni ya Clouds.
Jibu hilo la Ridhiwan... | kitaifa |
MANILA, PHILIPPINES RAIS wa Philippine, Rodrigo Duterte, ametishia kuwarusha viongozi mafisadi kutoka katika ndege angani, akisema ameshawahi kufanya hivyo kitambo. Duterte aliyasema hayo Jumanne wiki hii wakati akiwahutubia waathirika wa kimbunga katikati ya Philippines. “Kama wewe ni fisadi, nitakubeba kwa kutumia he... | kimataifa |
MASHIRIKISHO ya sanaa nchini yanatarajia kutoa tuzo ya heshima kwa viongozi mbalimbali akiwemo hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kutokana na mchango wake mkubwa katika tasnia hiyo.Pia yamepanga kumpa tuzo Rais John Magufuli na Rais wa Zanzibar, Dk Mohammed Shein kutokana na michango yao ya kufuata nyayo za M... | michezo |
UKITAZAMA kwa jicho la tatu, mwenendo wa mbio za marathon za kuwania ubingwa kwenye Ligi Kuu ya England (EPL) kati ya Manchester City na Liverpool, ilikuwa patashika ya nguo kuchanika, kwani City ilifanikiwa kubeba ubingwa huo kwa tofauti ya pointi moja dhidi ya mpinzani wake Liverpool.Mfano huo unaweza kuuleta Tanzan... | michezo |
RAMADHAN HASSAN -DODOMA MFUMUKO wa bei wa taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Juni 2020, umebaki kuwa asilimia 3.2 kama ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia Mei 2020. Hayo yalielezwa jana jijini hapa na Kaimu Mkurugenzi wa Takwimu na Sensa ya Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ruth Minja alipokuwa akizungumza na waandishi w... | uchumi |
KINSHASA, DRC Shirika la afya la kimataifa WHO, limetangaza kuwa hatari ya maambukizi ya ugonjwa wa Ebola kuzidi kusambaa na kiwango chake kiko juu zaidi miongoni mwa wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. WHO limeeleza kuwa vyanzo vya maambuziko ya ugonjwa wa Ebola vimeongezeka na sasa njia za usafiri na shughu... | kimataifa |
WATU wawili wanaodaiwa kuwa majambazi wamefariki dunia kwa kupigwa risasi na wenzao, baada ya kutaka kuwatoroka askari wakati wa operesheni ya kuwasaka majambazi mkoani Shinyanga.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Saimon Haule alithibitisha hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari. Alieleza kuwa mauaji hayo ya... | kitaifa |
Na MWANDIHI WETU, DAR ES SALAAM WAKAZI wa Kata za Kivule na Msongola wilayani Ilala mkoani Dar es Salaam waliovunjiwa nyumba zao wamemwomba Rais Dk. John Magufuli kuwatembelea kwenye makazi yao ili wamweleze unyama waliofanyiwa na kikundi kinachojiita Umoja wa Kikristo Tanzania (UVIKIUTA). Wakazi hao zaidi ya 2000 ni m... | kitaifa |
MADRID, HISPANIA KOCHA wa klabu ya mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Real Madrid, Zinedine Zidane, ameweka wazi kuwa nyota wake, Cristiano Ronaldo na nahodha Sergio Ramos, wamemaliza tofauti zao. Uongozi wa klabu hiyo uliwakutanisha wachezaji hao juzi, kabla ya kuelekea katika mchezo wao dhidi ya Atletico M... | michezo |
WAZAZI wa wanafunzi wanaosoma Shule ya Sekondari ya Dodoma kwa kushirikiana na Bodi ya shule wamekubaliana kuchangishana Sh milioni 264.3 kujenga uzio kuzunguka shule.Uamuzi huo wa kujenga uzio, ulifikiwa katika kikao hicho, baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Tamisemi, Selemani Jafo kuagiza bodi hiyo wakati wa ma... | kitaifa |
Simba na Singano wamekuwa kwenye mgogoro kwa takriban wiki ya pili sasa, ambapo mchezaji huyo anadai kutaka kuondoka kwa vile amemaliza mkataba wake wa miaka miwili huku uongozi wa klabu yake ukisema bado mchezaji wake halali kwani alisaini mkataba wa miaka mitatu unaotarajiwa kumalizika mwakani.Taarifa ya TFF kwa vyo... | michezo |
TIMU ya Taifa ya Tanzania Bara U20 imefuzu nusu fainali ya mashindano ya CECAFA yanayochezwa nchini Uganda baada ya kuwafunga wenyeji Uganda, Hippos, kwa mabao 4-2 katika mchezo uwa robo fainali kwenye Uwanja wa Pece, Gulu. Tanzania Bara U20 inayonolewa na kocha Zuberi Katwila ilianza kuzifumania nyavu za wapinzani wa... | michezo |
['Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa, watoto wanne kati ya watano wenye umri wa miaka 11-17 duniani hawafanyi mazoezi ya viungo ya kutosha.', 'Shirika la afya duniani (WHO) limesema kuwa afya za watoto zinaharibiwa kutokana na ukosefu wa mazoezi hivyo kuathiri ukuaji wa ubongo na shughuli zao za ujuzi kupungua uwezo.', '... | michezo |
NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Simba umetangaza kamati maalumu ambayo imepewa jukumu la kutafuta mwekezaji atakayenunua asilimia 50 ya hisa ili kukamilisha azma ya klabu hiyo kujiendesha kisasa. Hatua hiyo inatokana na klabu hiyo kubadili mfumo wake wa uendeshaji kutoka ule wa wanachama uliodumu kwa miaka mingi hadi kuwa w... | michezo |
Kiungo wa zamani wa Yanga Salvatory Edward ameingilia kati suala la kipa timu yake hiyo ya zamani Claus Kindoki.Kindoki aliyeletwa Yanga na kocha wa timu hiyo Mwinyi Zahera amekuwa akishutumiwa na mashabiki wa timu hiyo kutokana na kiwango kibovu anachoonyesha tangu alipojiunga na timu hiyo akitoka Jamhuri ya Kidemokr... | michezo |
WATU watatu wamekufa na wawili wamejeruhiwa na kulazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru, baada ya kufukiwa na kifusi kwenye machimbo ya moramu.Machimbo hayo yanayotumika kwa ajili ya shughuli za ujenzi, yapo eneo la Moivaro katika Kata ya Moshono jijini hapa.Tukio hilo limetokea umbali wa kilometa nane... | kitaifa |
Na ZAINAB IDDY-DAR ES SALAAM
TIMU ya taifa ya vijana walio chini ya miaka 17, Serengeti Boys, leo inarusha karata yake muhimu dhidi ya Niger katika mchezo wa Kombe la Afrika kwa vijana nchini Gabon.
Mchezo huo utafanyika katika Uwanja wa Port Gentil mjini Port Gentil, ambapo kikosi hicho kikiwa kimevuna poibn... | michezo |
Katika mechi hiyo Simba ililazimika kusawazisha dakika 10 kabla ya kumalizika mchezo kupitia kwa Brian Majwega baada ya Mwadui kuongoza kwa karibu muda wote wa mchezo kwa bao lililofungwa na Nizar Khalfan.Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya mtandao jana, Kerr alisema anajua mashabiki wa timu hiyo wanatamani kushind... | michezo |
Na NORA DAMIAN-DAR ES SALAAM
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimesema haki ya uhuru wa kujieleza na kukusanyika iko shakani, kutokana na kuwapo kwa udhaifu katika sheria mbalimbali.
Hapa nchini uhuru wa kujieleza unalindwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 18 na... | kitaifa |
MWANDISHI WETU WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amepokea hundi ya Sh bilioni 1.1 kutoka Kampuni ya Uchimbaji Madini Geita (GGML) ili kukabiliana na mapambano dhidi ya maambukizi ya corona. Akipokea hundi hiyo, Ummy alitoa wito kwa viwanda vya ndani kuchangamkia fursa za uzalisha... | afya |
KIBALI cha kukariri kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora, kimeleta kizaazaa na kusababisha wanafunzi 11 wa kidato cha nne kutolewa chumba cha mitihani na kuingizwa katika karandinga na kupelekwa kituo cha polisi.Tukio hilo lilitokea Ijumaa saa 2.15 asubuhi katika shule hiyo ambay... | kitaifa |
EVANS MAGEGE N LEONARD MANG’OHA-DAR ES SALAAM KANISA Katoliki nchini limewaelekeza waumini wake kufunga, kufanya hija, mikesha na maombi maalumu kwa lengo la kuombea mvua. Pamoja na hilo, kanisa hilo limewaelekeza viongozi wake kuadhimisha misa kwa lengo hilo hilo. Maelekezo hayo yametolewa na Mwenyekiti wa Baraza la M... | kitaifa |
ENDAPO ningembiwa kitu gani nikibadilishe kwenye tasnia ya muziki nchini basi ningebadilisha upepo wa Bongo Fleva uende sawa na muziki wa Dansi, muziki mama uliozaa aina zote za miziki unazozisikililiza.
Miaka ya 80 wakati haijulikana kama kuna muziki utazaliwa unaoitwa Bongo Fleva, muziki wa Dansi ulikamata se... | burudani |
HISTORIA ya aina yake imeandikwa katika sherehe za miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara na miaka 57 ya Jamhuri, zilizofanyika kwa mara ya kwanza katika Kanda ya Ziwa, na mkoani Mwanza.Kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza jana, uwanja huo na maeneo ya jirani vikiwamo Viwanja vya Furahisha, kuliandikwa historia kuto... | kitaifa |
Na NORA DAMIAN – DAR ES SALAAM WAKATI mchakato wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuwapata wagombea watakaopeperusha bendera ya chama hicho kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba ukitarajiwa kuanza kesho, joto linaonekana kuanza kupanda. Katika uchaguzi wa mwaka huu, mchuano mkali unatarajiwa kuwa ndani ya chama haswa kwenye nafasi... | kitaifa |
Na ASHA BANI – Dar es Salaam
WACHIMBAJI, wauzaji na wasafirishaji wadogo wa madini, wamemwomba Rais Dk. John Magufuli kuondoa zuio la kusafirisha mchanga wenye madini alilolitoa wiki iliyopita, baada ya kutembelea Bandari ya Dar es Salaam.
Pia wachimbaji hao wamesikitishwa na hatua ya watendaji kutoka Wizar... | kitaifa |
MANCHESTER, ENGLAND STAA wa mabingwa wa Ligi Kuu nchini England, Manchester City, Leroy Sane, ameweka wazi kuwa hana tatizo na kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani, Joachim Low, baada ya kumwacha kwenye michuano ya Kombe la Dunia. Mshambuliaji huyo wa pembeni alitikisa vyombo vya habari siku chache kabla ya kuanza kwa ... | michezo |
ABDUCADO EMMANUEL NA MITANDAO DIMBA la White Hart Lane linatarajia kuwaka moto kesho saa 9.00 alasiri kwa mchezo wa watani wa jadi wa jiji la London ‘London Derby’, wakati wenyeji Tottenham Hotspur watakapoikaribisha Chelsea katika Ligi Kuu England. Kuelekea mchezo huo, Kocha wa Tottenham, Mauricio Pochettino, ameanza ... | michezo |
Na Eliya Mboneya, Arusha Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu(AfCHPR), imesema Mahakama za ndani Tanzania katika kesi ya kubaka na kulawiti iliyokuwa inamkabili mwanamuziki Nguza Viking (Babu Seya) na mwanawe Johnson Nguza (Papii Kocha) zilitenda haki kwa kiwango kikubwa na kwa upande mwingine zilikiukwa. ... | kitaifa |
Na Florence Sanawa, Mtwara Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mtwara Mjini (MTUWASA), imeanzisha utaratibu mpya ya kulipia madeni yake kwa njia ya elektroniki kupitia mtandao wa simu za mkononi (NMB Mobile) ili kurahisisha ukusanyaji madeni katika Manispaa ya Mtwara Mikindani. Akizungumza na na waandishi wa ha... | kitaifa |
KLABU ya Yanga imewatuliza mashabiki wake kufuatia kutolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikisema kazi haijaisha wanajipanga upya kwa ajili ya Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho Afrika. Yanga imetolewa na Zesco United ya Zambia kwa jumla ya mabao 3-2, wakitoka sare nyumbani ya bao 1-1 na kufungwa ugenin... | michezo |
KOCHA wa AFC Leopards Casa Mbungo ameondoka klabuni hapo baada ya kusitisha mkataba wake. Kocha huyo mnyarwanda jana alikwenda mazoezini na kuwaaga wachezaji na wafanyakazi wenzake.“Nitawakumbuka, nitaikumbuka Kenya. Tafadhali endeleeni kufanya kazi kwa bidii, hamuwezi kujua kitakachokuja mbele,” Mbungo aliwaambia wac... | michezo |
Mwenyekiti wa Shiwata, Cassim Taalib alisema jana kuwa kikao cha Kamati Utendaji ya Mtandao huo kilichoketi juzi kilifikia uamuzi huo baada ya kufuatilia kwa karibu mafanikio ya Samatta akiwa na timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ na klabu yake ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na kufanya viz... | michezo |
MKUU wa Wilaya ya Chemba, Saimon Odunga amesema kesho watazindua utaratibu wa ugawaji wa vitambulisho vya wajasiriamali baada ya kupitisha vigezo ambavyo wanaona wanaweza kupata wajasiriamali.Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu, Odunga alisema sifa ambazo zimewekwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekuwa n... | kitaifa |
Na BADI MCHOMOLO
UKIWA unakumbwa na msongo wa mawazo mara kwa mara unaweza kufanya mambo ambayo utakuja kuyajutia katika maisha yao kama utashindwa kuwa makini na kufanya maamuzi sahihi juu ya mawazo ambayo yanakusumbua.
Wadau wengi wa muziki duniani waliguswa na kifo cha staa wa muziki wa Pop nchini Marekan... | burudani |
MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri zote mkoani humo ifi kapo Juni 30, mwaka huu, wawe wamekamilisha ununuzi wa mashine za kielektroniki za kukusanyia mapato.Akizungumza katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC), Dk Mahenge alisema halmashauri zote saba zinatakiwa k... | uchumi |
MWAMVITA MTANDA-DAR ES SALAAM BAADA ya Simba kupata ushindi wa mabao 2-1 katika
mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambao umewapa
nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Patrick
Aussems, amesema atapambana kuhakikisha kikosi chake kinachukua ubingwa wa
Afrika. Simba... | michezo |
Lulu Ringo, Dar es Salaam Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera amesema msimu huu wa 2018/2019 ukimalizika ataachana na timu hiyo kutokana na washabiki, wanachama wa klabu hiyo kushindwa kujitolea kuisaidia timu yao. Zahera ameiambia Mtanzania Digital kwamba anashangaa kuona Yanga ikijiita timu ya wananchi na ye... | michezo |
MANCHESTER, ENGLAND NAHODHA wa klabu ya Manchester United, Wayne Rooney, amedai kwamba wachezaji wanapaswa kulaumiwa na sio kocha wao, Van Gaal. Mshambuliaji huyo amesisitiza kwamba, wachezaji hawachezi kulingana na majukumu yao hivyo lawama anatupiwa kocha badala yao ambao wanatakiwa kuonesha uwezo wao kwa lengo la ku... | michezo |
Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA MWANASIASA Mkongwe nchini na Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa, John Shibuda amewataka waliopokea fedha za mgao wa Escrow kuzirejesha. Vilevile alimwomba Rais Dk.John Magufuli awasamehe. Shibuda ambaye amewahi kuwa Mbunge wa Maswa Magharibi na kwa sasa ni Katibu Mkuu wa Chama cha Ada ... | kitaifa |
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Dismas Ten amerusha kijembe kwa watani wao jadi Simba kufuatia usajili wa beki Kennedy Wilson Juma kutoka Singida United. Jana kupitia akaunti yao rasmi, klabu ya Simba ilitangaza umsajili beki huyo ambaye ana sifa ya matumizi makubwa ya nguvu awapo uwanjani kutokana ... | michezo |
WAKATI kocha wa Yanga SC, Charles Mkwasa, akiendelea kutupa vijembe vya kuwafunga wapinzani wao Simba SC kwenye mchezo wao wa mwishoni mwa wiki hii, kikosi hicho leo kimetamba kuendeleza makali yake dhidi ya Biashara United katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.Yanga wanaingia kweny... | michezo |
MKUU wa Jeshi la Polis Nchini (IGP), Simon Sirro amewang’oa rasmi wakuu wa Polisi wa mikoa watatu (RPC), walioachishwa kushika nyadhifa zao na Waziri wa Mambo ya Ndani na Nchi, Kangi Lugola.Hivi karibuni Lugola alitangaza kuwa wakuu hao wa Polisi, wanatakiwa kuachia wadhifa wao kutokana na sababu tatu kuu, ambazo alis... | kitaifa |
Na UPENDO MOSHA, MOSHI BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, limepitisha sheria mbili za kudhibiti utumiaji wa mifuko ya plastiki pamoja na kudhibiti ufungaji wa mazao kwa mtindo wa lumbesa. Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika jana mjini Moshi wakati wa mj... | kitaifa |
NA MOHAMED KASSARA-DAR ES SALAAM MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili Simba, Zakaria Hanspope, amesema kwa sasa hayupo tayari kukaimu nafasi ya raisi wa klabu hiyo, Evans Aveva na Makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ kutokana na kukabiliwa na majukumu mengi. Aveva na Makamu wake Kaburu, Juni 28, mwaka huu walipandishwa kiz... | michezo |
MOSCOW, URUSI UFARANSA wamefanikiwa kuingia hatua ya fainali kwenye michuano ya Kombe la Dunia nchini Urusi, baada ya juzi kushinda bao 1-0 dhidi ya Ubelgiji. Ushindani ulikuwa wa hali ya juu katika mchezo huo kutokana na ubora wa kila timu, lakini Ufaransa imeweza kuwazidi wapinzani kutokana na vitu vifuatavyo. Mlind... | michezo |
TRIPOLI, LIBYA MAELFU ya wananchi nchini Libya wamefanya maandamano katika mji mkuu wa nchi hiyo wa Tripoli wakiwa wamevalia vizibao vya njano kama wanavyofanya washiriki wa maandamano ya vizibao vya njano kupinga siasa za kiuchumi za serikali ya Ufaransa, ambapo nao wamelaani mienendo hasi ya Serikali ya Rais Emmanuel... | kimataifa |
CHUO Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kinatarajia kuanza kutoa Mitihani ya Kimataifa ya Ujuzi wa lugha ya Kiswahili (MKUKi) kuanzia mapema mwakani.Hayo yalibainishwa jana jijini hapa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Leonard Akwilapo, alipokuwa akizungumzia mpango huo ambao pia umelenga kukuza... | kitaifa |
MAREGESI PAUL Na
RAMADHAN HASSAN
-DODOMA
MBUNGE wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema), amesema wananchi wamewageuza wabunge wa Tanzania na kuwa kama mashine za kutolea fedha (ATM) na Vyama vya Kuweka na Kukopa (SACCOS).
Kutokana na hali hiyo, amesema kuna haja Serikali kuboresha mafao yao ili yaendane na ... | kitaifa |
BAADHI ya wachambuzi na makocha wa soka nchini wametaja timu tano zinazoweza kufika mbali kwenye fainali za Mataifa ya Afrika zinazoendelea nchini Misri, huku wenyeji wakipewa asilimia 100.Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti jana, wachambuzi hao Ally Mayai, Dominick Salamba na Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ kila ... | michezo |
Kikwete alitoa agizo hilo katika hafla ya kumuaga iliyoandaliwa na wasanii kutokana na mchango wake mkubwa katika tasnia ya sanaa.Katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam, Kikwete alisema kuwa Cosota inatakiwa kuhakikisha inadhibiti wizi wa kazi za wasanii nchini kutokana na watu weng... | michezo |
Kulwa
Mzee, Dar es Salaam Msanii wa Filamu nchini, Wema Sepetu aliyekuwa
mahabusu katika Gereza la Segerea ameachiwa kwa onyo na dhamana yake
inaendelea. Uamuzi huo umetolewa leo Jumatatu Juni 24, saa
nne asubuhi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi, Maira
Kasonde. Akitoa uamuzi wa aidha Wema a... | kitaifa |
Ramadhan Hassan -Dodoma SERIKALI imesema bado kuna tatizo la matumizi makubwa ya bangi nchini ambapo mwaka 2015 hadi Juni, 2020, kilo 188,489.93 za bangi zimekamatwa. Hayo yalielezwa jana jijini hapa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana, Sera na Watu wenye ulemavu, Jenista Mhagama, wakati aki... | afya |
WASHINGTON, MAREKANI RAIS wa Marekani, Donald Trump amesema ni ‘’ ni heshima ‘’Marekani ina idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya corona duniani. ‘’Ninalitazama suala hili kama heshima fulani, kama jambo zuri kwasababu inamaanisha kuwa vipimo vyetu viko vizuri,’’ alieleza akiwa Ikulu ya Marekani. Marekani ina wat... | kimataifa |
LONDON, ENGLAND UONGOZI wa timu ya Tottenham umethibitisha utaikosa huduma ya mlinda mlango
wake Hugo Lloris hadi 2020 baada ya kupata tatizo la kugeuka kiwiko kwenye
mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Brighton mwishoni mwa wiki iliopita. Katika mchezo huo, Tottenham ambao walikuwa ugenini walikubali kichapo cha
mabao... | michezo |
Na NORA DAMIAN-DAR ES SALAAM
SERIKALI inapoteza dola za Marekani milioni 100 kila mwaka kutokana na kuagiza dawa kutoka nje ya nchi.
Viwanda vya dawa vilivyopo nchini ni 13 tu ambapo uwezo wake wa kuzalisha ni asilimia 20 ya dawa zote zinazohitajika nchini.
Hayo yalisemwa juzi na Mfamasia wa Wizara ya Afya... | kitaifa |
Na MAREGESI PAUL – DODOMA BOMOABOMOA inayoendelea nchini kwa wananchi waliojenga katika maeneo ya Shirika la Reli Tanzania (TRC), imewakera baadhi ya wabunge. Wabunge hao walionyesha hali hiyo bungeni jana wakati walipokuwa wakichangia Muswada wa Sheria ya Reli ya Mwaka 2017, uliowasilishwa bungeni na Waziri wa Ujenzi... | kitaifa |
Na RAMADHAN LIBENANGA-MOROGORO
WAFUGAJI wilayani Mvomero Mkoa wa Morogoro, wamesema wamekuwa wakitumia fedha nyingi kununua mihtasari ya vikao vya vijiji ili kuzionyesha mamlaka mbalimbali jinsi walivyoruhusiwa kumiliki ardhi waliyonayo.
Hayo yalielezwa jana na mchungaji Joseph Sepuke, alipokuwa akizungumza kwenye mku... | kitaifa |
Mwandishi Wetu,Dar es Salaam ZAIDI ya wafanyabiashara 2000 katika mkoa wa kodi wa Ilala wamepatiwa elimu ya kodi inayoendelea katika mikoa mbalimbali nchini.Mamlaka hiyo imekuwa na ikifanya kampeni ya elimu ya kodi mara kwa mara kwa kuwafata wafanyabiashara kwenye biashara zao (mlango kwa mlango). Akizungumzai zoezi hi... | uchumi |
Na Said Ameir, MAELEZO KUWAPATIA wananchi dawa zenye viwango bora, salama na ufanisi ni moja kati ya malengo makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuimarisha afya za watu. Pamoja na lengo hilo, utekelezaji wake mbali ya kukabiliwa na chagamoto za kibajeti, changamoto nyingine kubwa ni upungufu wa wataalamu wa uk... | afya |
MWILI wa binadamu na viumbe wengine kama vile wanyama, una mfumo unaosaidia kujilinda dhidi ya magonjwa mbalimbali. Mfumo huu wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa kwa kitaalamu huitwa ‘Immune system.’ Pamoja na mwili kuwa na mfumo wa kujilinda dhidi ya magonjwa, kuna nyakati ambazo kinga hii ya mwili inakuwa haijakomaa... | afya |
Na WAANDISHI WETU – ZANZIBAR/DAR ES SALAAM
RAIS wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, amesema iwapo Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) litaikatia umeme Zanzibar kutokana na deni wanalodaiwa, wataweza kurudi katika matumizi ya asili ambayo ni kutumia vibatari kupata mwanga.
Dk. Shein aliyasema hayo mara baada ... | kitaifa |
Alitoa pongezi hizo alipozindua rasmi hatua ya benki hiyo, Mwalimu Commercial Bank (MCB) kujiorodhesha DSE mwishoni mwa wiki Dar es Salaam tayari kwa kuanza kuuza hisa zake. “Soko la hisa ni njia mpya ya kuwakwamua walimu kiuchumi na kuzidi kujiendeleza kimaisha,” alisema Majaliwa.Alisema Serikali ya Awamu ya Tano ime... | uchumi |
Na NORA DAMIAN-DAR ES SALAAM TEKLA (si jina lake halisi), ni mwalimu katika shule moja ya msingi jijini Dar es Salaam. Katika harakati za kutafuta maisha amekumbana na changamoto nyingi ambazo kama si mama yake kupambana huenda leo angekuwa na maisha mabaya zaidi. Tekla anasema alikuwa akiishi na mama na baba yake wa... | kitaifa |
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Dk Rehema Nchimbi wakati alipokutana na Watumishi wa Halmashuri ya Mji wa Makambako, alisema mradi wa Liganga na Mchuchuma utatoa ajira zaidi ya 30,000, zikiwepo za wazawa na wageni.Aliwataka watumishi wa Halmashauri ya Mji Makambako hasa sekta ya ardhi kuhakikisha wanaweka mipango mizuri ya ma... | uchumi |
MABINGWA wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara, Simba, wameialika Asante Kotoko ya Ghana kucheza nayo mechi ya kirafiki katika kilele cha maadhimisho ya Simba Day Agosti 8, mwaka huu.Simba hufanya tamasha hilo Agosti ya kila mwaka ambapo kabla ya kufikia kilele tarehe nane, hufanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwa ni pam... | michezo |
WIKI iliyopita, nilianza makala haya yanayolenga kuwahimiza Watanzania wenzangu kumsaidia Rais wetu, John Magufuli, kutekeleza ahadi yake kubwa kwa Watanzania ya kuipeleka nchi katika uchumi wa kati ifi kapo mwaka 2025.Baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, hatuna rais mwingine zaidi ya Magufuli aliyechaguliwa kidemokr... | kitaifa |
Subsets and Splits
No community queries yet
The top public SQL queries from the community will appear here once available.