content
stringlengths
1k
24.2k
category
stringclasses
6 values
WAZIRI wa Madini, Doto Biteko amewaonya wamiliki wa migodi ya tanzanite Mirerani kwa fedha kidogo wanazochangia za kodi, na kusisitiza kuwa wasipolipa kodi hiyo, rungu litakapowafikia halitowaacha salama.Aidha, waziri huyo amebainisha kuwa mpaka sasa serikali imefuta leseni 12,000 za migodi baada ya kushindwa kulipa k...
uchumi
SERIKALI ya Kenya inatarajia kuanza utekelezaji wa sheria ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu uingizaji wa magari kutoka nje.Sheria ya jumuiya hiyo inazitaka nchi wanachama, kutoingiza magari kutoka nje yenye umri kuanzia miaka mitano na kuendelea. Wakati Kenya ikichukua maamuzi hayo, Tanzania inaendelea kutekeleza ...
kitaifa
Meneja wa kiwanda hicho, Pratap Disodya aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa kiwanda hicho hakina sababu ya kuficha sukari kwa kuwa kina uwezo wa kuzalisha tani 300 hadi 500 kwa siku.Alisema pamoja na uzalishaji huo unaochangiwa na upungufu wa miwa kutoka kwa wakulima, kiwanda hicho pia kinalazimika kufungwa kila ...
uchumi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli amewataka watanzania kuendelea kuishi katika umoja na mshikamano kama nguzo kuu ya maendeleo nchini.Rais ametoa wito huo leo Jijini Dar es Salaam katika hafla ya mashindano maalumu ya usomaji wa Quran barani Afrika  yanayoandaliwa na taasisi ya Al-Hikma yaliyo...
kitaifa
Mfumo huo ulitambulishwa jana kwa mawakala wa forodha na unatarajiwa kuanza kutumika Machi mosi mwaka huu, sambamba na mfumo unaotumika awali wa ASYCUDA, unatarajiwa kuachwa kutumika kuanzia Aprili mwaka huu baada ya kuonekana kuwa na mapungufu mengi.Naibu Kamishna Uboreshaji na Vihatarishi wa TRA, Bellium Silaa akifu...
uchumi
BAADA ya kuwa katika hali ya mvutano na Rais Uhuru Kenyatta kwa muda mrefu, Gavana wa Mombasa, Hassan Joho anaonekana kuwa karibu na kiongozi huyo wa nchi tangu mshikamano wa nchi ulipoasisiwa na Uhuru na Raila Odinga.Katika ziara ya hivi karibuni ya Rais Uhuru Kenyatta huko Liwatoni katika Kaunti ya Mombasa ambapo al...
kitaifa
Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe ameanza kazi kwa kuhudhuria kikao kazi cha uongozi wa juu wa wizara hiyo kuelezwa taswira na mwelekeo wa mamlaka hiyo ya Serikali.Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga ameongoza kikao hicho katika ofisi ndogo za wizara hiyo jijini Dar es Salaam.Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba na Kati...
kitaifa
KWA mara nyingine Zarina Hassan ‘Zari’ ambaye ni mzazi mwenza wa msanii Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz’ ameingia kwenye vichwa vya habari baada ya kila mara kumfi cha mpenzi wake mpya, hali iliyomfanya kukasirika baada ya watu kuhoji. Miezi mitatu iliyopita mjasiriamali huyo raia wa Uganda alitangaza kuingia kuwa kweny...
michezo
WAKATI binti wa miaka 17 aliyekuwa akifanya kazi za ndani jijini Dar es Salaam akieleza ukatili aliokuwa akifanyiwa na bosi wake, ikiwemo kuwekewa mwiko sehemu za siri hali inayosababisha asione siku zake (hedhi) kwa mwaka mmoja sasa, taasisi mbalimbali zimeelezwa kushangazwa na ukatili wa aina hiyo na kutaka hatua ka...
kitaifa
Mfumo huo mpya umetengenezwa katika namna inayowezesha wazee kupata mafao yao ya kila mwezi kupitia katika mashine za kutolea fedha (ATM), TigoPesa na M-Pesa, vituo vya mauzo na mitandao mingine.Akizungumza katika maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa (DITF) Ofisa Operesheni wa NSSF, Joyce Mruma alisema: “Wazee weny...
uchumi
MWANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Ardhi, Anna Mwaisumo (23) na mpenzi wake Samson Kisuguta (28), wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka manne ikiwemo ya kulawiti na kusambaza picha za ngono kwenye mtandao wa kijamii wa WhatsApp.Mwaisomo ambaye makazi yake ni kwenye Hosteli za Chuo Kik...
kitaifa
Timu hizo za ukanda wa Afrika Mashariki zilifuzu hatua hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kushinda mechi zake za marudiano. Fainali za michuano hiyo zimepangwa kufanyika mapema mwakani nchini Niger.Tanzania, Ngorongoro Heroes imefuzu hatua hiyo kwa ushindi wa mikwaju ya penalti 6-5 katika mechi iliyochezwa Kins...
michezo
MADEREVA wa bodaboda kutoka kata nane za Manispaa ya Kinondoni wamepewa msaada wa kofia ngumu na Kampuni ya Mcheza ikiwa ni sehemu ya kutoa hamasa ya kujikinga na ajali za barabarani wao na abiria.Akizungumza kwenye Viwanja vya Biafra baada ya kukabidhiwa Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Madereva wa Bajaji na Bodaboda Ki...
michezo
PEP Guardiola amesema ni wendawazimu na upuuzi kwa Manchester City kufi kiria kuhusu kutwaa taji licha ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Burnley juzi usiku.City imejikongoja mpaka kufikia tofauti ya pointi nane dhidi ya vinara Liverpool, shukrani kwa Gabriel Jesus aliyefunga mabao mawili na mabao mengine kutoka kwa Rod...
michezo
['Mchezaji Bruno Fernandes ameanza mchakato wa kuhamia Old Trafford. Nyota huyo wa miaka 24 anayecheza safu ya kati ya Sporting Lisbon na Ureno anatarajiwa kwenda Manchester kufanya vipimo vya afya. (Sport Witness)', 'Red Devils wanamlenga mlinzi wa Atletico Madrid na Uhispania Saul Niguez, 24, kuchukua nafasi ya Paul ...
michezo
KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema baridi inawapa changamoto, lakini anaamini watazoea na kuwa fiti kabla ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa Afrika dhidi ya Al Ahly unaotarajiwa kuchezwa kesho Uwanja wa Borg El Arab.Kwa mujibu wa taarifa kutoka Alexandria, Misri, baridi imekuwa ikiisumbua Simba wakati wa mazoe...
kitaifa
OFISI ya Waziri Mkuu chini ya Baraza la Taifa la Biashara, kupitia Mradi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji, unaotekelezwa katika mikoa ya Kigoma na Dodoma, umeboresha mazingira ya biashara na uwekezaji katika mikoa hiyo kwa kutumia kiasi cha Sh bilioni 16 hadi kufi kia mwezi huu.Mradi huo ambao utekeleza...
kitaifa
Kaimu Kamishina Mkuu wa TRA, Rished Bade, alisema hayo jana jijini hapa alipozungumza na waandishi wa habari.Wakati kukiwa na mgomo nchi nzima dhidi ya matumizi ya mashine hizo, Bade alisisitiza kuwa wakati wa kufanya biashara bila ya kulipa kodi halali umepitwa na wakati na kila mmoja anapaswa kulipa kodi kutokana na...
uchumi
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kushiriki mbio za 18 za Kilimanjaro zitakazofanyika Machi mwakani, Mwakyembe pia aliwataka wanariadha wa Tanzania kufanya maandalizi ya uhakika ili kuhakikisha wanafanya vizuri katika mbio hizo, ambazo ni kub...
michezo
MKAZI wa Mhunze wilayani Kishapu Mkoa wa Shinyanga, Raphael Martine (34), anashikiliwa na Polisi akituhumiwa kumuua Shija Mahoiga (45), kwa  kumpiga kwa chuma kichwani, mikononi, na sehemu za mbavu.Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Richard Abwao amethibitisha mauaji hayo ya juzi saa tisa usiku, akisema mtuhumiwa alidai kwend...
kitaifa
Akizungumza hivi karibuni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba Tanzania (TCB) , Gabriel Mwalo, amesema kuna faida nyingi katika kilimo cha mkataba lakini kukosekana kwa usimamizi na kutoungwa mkono vya kutosha kutoka serikalini kunawafanya wawekezaji kutochangia fedha nyingi zinazohitajika.Semina hiyo ilikuwa ya kuw...
uchumi
MATUMIZI ya pombe yanatarajiwa kuongezeka duniani kwa muongo ujao kutokana na nchi mbalimbali kutotelekeza ahadi ya kuwalinda wananchi wao kutoka katika matumizi mabaya ya vilevi.Tafiti zinaeleza kuongezeka kwa matumizi ya pombe kimataifa yanachangia ongezeko la matumizi hayo ya pombe kwa nchi zenye vipato vya chini. ...
kitaifa
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Awadh Massawe, aliyasema hayo mjini hapa hivi karibuni kuwa, mawakala wa mizigo wana mchango mkubwa wa kujenga mazingira bora ya biashara na kuifanya nchi kuwa shindani barani Afrika.“Tunazidi kuimarisha huduma bandarini, lakini pia ni muhimu wakala wa mizigo...
uchumi
MABINGWA wa kihistoria Yanga, wamepunguzwa kasi na Mbeya City baada ya kutoka suluhu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa katika Uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.Mchezo huo ulianza kwa kasi kwa Yanga kutawala sehemu ya kiungo na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga mabao huku wakilisakama lango la wapinzan...
michezo
Katika swali lake, Owenya, alitaka kufahamu ATCL inamiliki ndege ngapi na kati ya hizo, ni ngapi zimekodishwa na zinafanya safari kwenda wapi.Baada ya kujibiwa kwamba ndege inayomilikiwa na ATCL ni moja, Owenya alisema ni aibu kwa shirika kuwa na ndege moja wakati liliwahi kumiliki ndege saba.Ili kuondoa aibu hiyo, Mb...
uchumi
Wachinjaji na wauzaji wanakwepa kushusha mifugo yao katika mnada wa Pugu kwa kutokuwa na vibali vya maeneo watokako na kusababisha ukosefu wa mapato kwa Serikali.Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Maria Mashingo aliyasema hayo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika eneo la Vingunguti na kuzungum...
uchumi
Lipuli iliyopanda Ligi Kuu msimu huu, ilikuwa ya kwanza kupata bao katika dakika ya 45 kupitia kwa Seif Abdallah akiunganisha pasi ya Malimi Busungu kabla ya kuachia shuti lililojaa wavuni.Dakika tatu za nyongeza ziliitosha Yanga kusawazisha bao hilo kupitia kwa Donald Ngoma aliyeunganisha kwa kichwa mpira wa kona wa ...
michezo
MAKAMU wa Ris Samia Suluhu Hassan ameahidi viwanja vya kujengea nyumba kwa wachezaji wa timu ya soka ya Taifa ya wanawake, Twiga Stars endapo watafuzu michezo ya Olimpiki 2020, Japan.Twiga Stars ipo kwenye kinyang’anyiro cha kufuzu michuano hiyo, ambapo juzi ilicheza na Congo DR kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam na...
michezo
TIMU ya taifa ya riadha itakayoshiriki mbio za dunia za nyika zitakazofanyika Aarhus, Denmark, Machi 30 imetamba kurudi na medali kutoka katika mashindano hayo.Hayo yalisemwa jana na nahodha wa timu hiyo, Marco Sylivestre baada ya kukabidhiwa bendera ya taifa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harris...
michezo
Mkazi huyo wa Dodoma aliyekabidhiwa gari ni Ivan Mbogambi anayetoka Kongwa. Akizungumza katika hafla ya makabidiano ya gari yake, Mbogambi alisema: “Nina furaha kubwa leo kwani nimeweza kuwa mmoja wa watu wanaomiliki gari wilayani kwetu.Mimi ni mkulima wa hali ya chini leo hii Airtel imeniwezesha kubadili maisha yangu...
uchumi
SERIKALI imeanza mchakato wa kupata wazabuni wa ndani na nje ya nchi wa kubangua korosho kwa lengo la kuharakisha uandaliwaji wake tayari kwa mauzo.Hivi karibuni Rais John Magufuli alitangaza nyongeza ya bei ya kununulia zao hilo kufikia Sh 3,300 kwa kilo huku akiliagiza Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kuk...
uchumi
WILAYA ya Kongwa mkoani Dodoma imeanza mkakati wa kuongeza uzalishaji wa zao la alizeti katika msimu wa kilimo wa mwaka 2018/19.Mwenyekiti wa Baraza la Biashara wilayani humo, ambaye ni Mkuu wa Wilaya, Deogratias Ndejembi amesema hayo katika kikao cha baraza hilo.Ameongeza kuwa mkakati huo, utahusisha mnyororo wote wa...
uchumi
NYOTA ya uwekezaji katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), imeendelea kung’aa na itazidi kung’aa mwaka 2019.Ripoti ya Benki ya Biashara ya Rand (RMB) ya Afrika Kusini, imeonesha kuwa Afrika Mashariki itakuwa kitovu cha uwekezaji barani Afrika mwaka huu. Hii ni kutokana na juhudi za nchi wanachama wa jumuiya ...
kitaifa
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko amesema leo jijini Dar es Salaam kuwa, mauzo ya almasi hizo kutoka kampuni ya uchimbaji madini ya ‘Williamson Diamond Limited’ yalifanyika nchini Ubelgiji kati ya Februari 2 hadi 9 mwaka huu na kuhudhuriwa na baadhi ya maofisa kutoka wizara hiyo.Amesema, katika mnada huo, jumla ya K...
uchumi
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya wa Kisarawe Mussa Gama amesema, kufunguliwa jengo la kisasa la abiria kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam ni fursa kubwa ya uchumi kwa wilaya hiyo.Amesema, kufunguliwa kwa jengo hilo kutaongeza idadi ya watalii wanaoutumia hivyo...
uchumi
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga amesema maonesho ya kwanza ya viwanda mkoa wa Pwani mwaka uliopita yalikuwa na tija kubwa kwa wawekezaji wilayani humo.Amesema ofisini kwake kuwa, wilaya hiyo ilikuwa na washiriki wengi na wamejiandaa vizuri kushiriki maonesho ya mwaka huu yanayotarajiwa kufanyika kwa wiki mo...
uchumi
HALI ya uzazi wa mpango nchini bado iko nyuma, jambo ambalo linahitaji kuwekewa nguvu kubwa, imeelezwa. Akizungumza katika mkutano uliozikutanisha asasi za kiraia, Mkurugenzi wa Miradi wa Taasisi ya Afya Tanzania, Salvatory Hokororo alisema jamii bado haina elimu ya kutosha.“Kulingana na takwimu za Wizara ya Afya, Mae...
kitaifa
ASASI za Kiraia zimesema licha ya muswada wa Sheria wa vyama vya siasa kuwa na baadhi ya vipengele vizuri, kuna haja ya vile vyenye upungufu kufanyiwa marekebisho kabla ya Bunge kuupitisha.Viongozi wa asasi za kiraia walisema jana Dar es Salaam kuna haja ya wabunge kuupa muswada muda wa kutosha kuuchambua kwa kina kab...
kitaifa
EMMANUEL Amunike. Namuelewa kwenye namna nyingi za ufundishaji wake. Namuelewa kuwa ni kocha anayependa sana soka la mbinu na matokeo.Lakini leo ningependa kuelewa kile anachokifanya kwa kiungo wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto kwenye kikosi chake. Kama walivyo watu wengi ndivyo ilivyo kwa kocha Amunike. Anatambua kipa...
michezo
WAKATI kikosi cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania Bara Kilimanjaro Stars kikitarajiwa kuwakabili Kenya leo, Kocha Mkuu Juma Mgunda amesema hatowadharau wapinzani wake.Katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza michuano ya Chalenji ya Baraza la vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), Kenya ambao walikuwa mabin...
michezo
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imevitaka vyama vya siasa nchini kutopeleka malalamiko yao katika vyombo vya habari kuhusu masuala ya uchaguzi na badala yake viwasilishe hoja hizo katika Kamati za Maadili za Uchaguzi.Imesema haina mfumo wa kushughulikia malalamiko ya uchaguzi kupitia vyombo vya habari badala yake imet...
kitaifa
HOSTELI bubu katika maeneo ya vijijini zimetajwa kuwa ni moja ya chanzo cha mimba za utotoni katika Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.Sababu nyingine za mimba za utotoni ni wengi kutoka familia maskini hawana magodoro wanalalia mifuko ya salfeti au maboksi huku bajeti ya chakula ikiwa ndogo hali inayosababisha kuingia k...
kitaifa
Mkataba huo umeingiwa rasmi jana katika Uwanja wa Taifa na kushuhudiwa na wanachama kutokea klabu mbalimbali za mchezo huo jijini Dar es Salaam.Meneja wa Mauzo na Masoko wa TSN, Januarius Maganga amesema, kwa kuzingatia mkataba huo, TEJA itanufaka na huduma bora za habari kutokea gazeti la Sports Leo, kwa kuwa taarifa...
michezo
Hayo yalisema juzi na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda wakati akifungua kikao cha kazi kilichofanyika Dar es Salaam na kuwashirikisha viongozi wa wizara na wakuu wa taasisi zake.Alisema katika kipindi cha mwaka juzi, sekta hiyo ilikua kwa asilimia 8.2, ikilinganishwa na asilimia 7.8 mwaka 2011. Pia, m...
uchumi
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu msanii wa Bongo Movie, Wema Sepetu kulipa faini ya Sh milioni mbili au kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela, baada ya kutiwa hatiani kwa mashitaka ya kukutwa na kutumia dawa za kulevya aina ya bangi.Sababu zilizochangia Wema kutiwa hatiani ni kitendo cha kukiri mwenyewe kwa...
michezo
TIMU ya soka ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys leo inarusha kete yake ya pili kwenye michuano ya Afrika kwa kumenyana na Uganda kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.Mechi hiyo ya kundi A inatarajiwa kuwa ya vuta nikuvute kutokana na matokeo ya timu hizo katika mechi zilizopita ambapo zote zi...
michezo
HOSPITALI ya Benjamin Mkapa (BMH) iliyopo Dodoma inatarajia kuendesha kambi ya wiki mbili kwa ajili ya upasuaji wa matundu madogo (endoscopic surgery) kwa wanawake wenye matatizo ya uzazi na ngiri.Hayo yalielezwa jijini hapa na Daktari Bingwa wa magonjwa ya kinamama na uzazi katika hospitali hiyo, Dk Januarius Hinju. ...
kitaifa
SIKU ya jana ilikuwa ni siku ya huzuni na simanzi zilizotawala kwenye nyuso za waombolezaji waliofurika kwenye ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wa Chimwaga wakati wa kumuaga aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Egid Mubofu.Katika maombolezo hayo ambayo yalitanguliwa na ibada takatifu, waombolezaji walipa...
kitaifa
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi hundi tatu zenye thamani ya jumla ya Sh milioni 6 kwa vikundi vitatu vya vijana, Diwani wa kata hiyo, Saidi Nassoro alisema pesa hizo ni za Serikali ambazo zinatokana na kodi za wananchi hivyo kila mtu ana haki ya kupata.Alisema, iwapo pesa hizo zitarudi kwa wakati, kupitia vikao ...
uchumi
['Polisi wanaochunguza madai ya ubakaji dhidi ya mchezaji wa Brazil Neymar wamesema wametupilia mbali kesi hiyo.', 'Ofisi ya mwanasheria wa São Paulo imesema kesi hiyo imetupiliwa mbali kutokana na kukosekana ushahidi, lakini suala hilo litapelekwa kwa waendesha mashtaka kwa ajili ya uamuzi wa mwisho.', 'Uchunguzi uli...
michezo
KIWANGO cha ukatili wa kijinsia nchini Tanzania kimeongezeka huku mikoa nane ikitajwa kuongoza kwa ukatili dhidi ya watoto nchini. Mikoa iliyotajwa kuwa na kiwango kikubwa cha ukatili wa watoto ni Dar es Salaam, Mbeya, Mwanza, Simiyu, Arusha, Kilimanjaro, Tabora na Singida.Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa uz...
kitaifa
“NAIPONGEZA timu nzima ya Mkoa wa Arusha iliyobuni mtihani wa pamoja kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari hapa mkoani ambao sasa unasaidia wanafunzi kukuza vipaji vyao na kuwawezesha kuongeza ufaulu zaidi.”Ndivyo anavyosema Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo anapozungumza katika hafla ya uzinduzi wa mpango ...
kitaifa
MTOTO wa tembo mwenye umri wa chini ya mwaka mmoja aliyeokolewa baada ya kutumbukia na kunasa kwenye tope shimoni ndani ya Pori la Akiba la Lwafi wilayani Nkasi Mkoa wa Rukwa, anatibiwa katika kituo cha kupokea wanyamapori yatima cha Makoa Farm Vertinary clinic mkoani Kilimanjaro.Kituo hicho kipo Machame wilayani Hai ...
kitaifa
CHAMA cha Riadha nchini (RT), kimetoa baraka kwa wandaaji wa mbio za kujifurahisha Mbezi Fun Run zilizopangwa kufanyika Desemba Mos, jijini Dar es Salaam.Katibu Mkuu wa RT, Willihelmi Gudagudai amesema leo Alhamisi kuwa RT imetoa kibali kwa wandaaji hao baada ya kufuata taratibu zote."Tumewataka baada ya tamasha lao, ...
michezo
HAYAWI hayawi sasa yamekuwa, baada ya Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL), kupewa kibali rasmi cha kuanza safari za ndege zake kwenda nchini India.Akizungumza na Habarileo jana, Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Ladslaus Matindi alisema ni kweli wamepewa kibali cha kuanza safari za ndege zake nchini India, kilichotolewa na...
kitaifa
KAMATI ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma imeiagiza Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kuhakikisha inapeleka vifaa tiba na dawa katika vituo vya afya vilivyokamilika.Pia wauguzi na wataalamu wa afya, wametakiwa kutoa huduma kwa kuzingatia weledi, kama ambavyo kanuni za taaluma yao zinavyoelekeza.Agizo hilo lim...
kitaifa
TIMU ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inatarajiwa kucheza leo dhidi ya timu ya taifa ya Kenya ‘Harembee Stars’ mchezo wa kwanza wa kutafuta tiketi ya kufuzu fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan 2020) utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Mchezo huo ni muhimu kwa Stars kuhakikisha inatumia vyem...
michezo
Benki hiyo iliyoanza kutoa huduma zake Agosti,1997 ikiwa na tawi moja jijini Dar es Salaam, kwa sasa ina jumla ya matawi 30 hapa nchini na matawi saba nje ya nchi huku rasilimali yake ikitajwa kuwa na thamani ya Sh trilioni 1.1 hadi kufikia Juni mwaka huu.Akizungumza juzi kwenye hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya ...
uchumi
Uwezeshaji huo upo katika kuwapatia elimu ya ujasiriamali pamoja na kuwawezesha vitendea kazi vya kisasa ili waweze kufikia ndoto zao.Mikoa iliyofikiwa na Airtel kupitia mradi huo wa jamii ni pamoja na Dar es Salaam, Morogoro, Lindi, Kagera, Manyara na Dodoma.Mkuu wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano alisema mik...
uchumi
IMEELEZWA kuwa asilimia 85 ya upungufu wa nguvu za kiume kwa wanaume unatokana na magonjwa ya moyo na kisukari, hivyo Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imeamua kuleta dawa za kurejesha nguvu hizo wakati wanaume wakiendelea na matibabu ya vishawishi.Dawa hizo zinatolewa katika Viwanja vya Maonesho vya Mwalimu Ju...
kitaifa
Akizungumza na wakulima na wananchi, Dk Shein alisema karafuu ndio alama ya Zanzibar, hivyo ni wajibu wa wananchi kutunza na kuenzi zao hilo kwa manufaa ya nchi na wananchi wake.Alisema serikali imefanya mabadiliko makubwa ya maendeleo ya zao hilo, ikiwemo kufanya mabadiliko katika Shirika la Biashara la Taifa Zanziba...
uchumi
KIKOSI cha timu ya soka ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 23, leo kiko ugenini mjini Bujumbura kucheza na wenyeji wao Burundi katika mechi ya kuwania kufuzu michuano ya Afrika ‘Afcon’ kwa vijana wa umri huo.Akizungumza saa chache kabla ya kuondoka jana, kocha msaidizi wa timu hiyo Bakari Shime alisema timu hiy...
michezo
['Barcelona wamesitisha jaribio lao la kutaka kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil Neymarkutoka Paris Saint-Germain hadi msimu ujao. (ESPN)', 'Mazungumzo kati ya vilabu hivyo yalivunjika baada ya PSG kulegeza masharti yao licha ya Neymar kujitolea kulipa £17.7m kufikia makubaliano ya usajili wake. (Sky Sports)...
michezo
KOCHA wa Simba, Patrick Aussems amesema walilazimika kubadili mbinu za uchezaji ili kupata matokeo mazuri katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya African Lyon, ambao walishinda 3-0 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.Akizungumza baada ya mchezo huo, Aussems alisema uwanja haukuwa rafiki ndio maana walikuja na mbinu ...
michezo
KIPA wa Simba na timu ya taifa, Taifa Stars, Aishi Manula, amesema Benno Kakolanya hakwenda Simba kushindana naye ila kushirikiana kuifikisha klabu hiyo inapotaka kufika.Kakolanya amejiunga Simba SC msimu huu akitokea Yanga, hivyo kwa sasa makipa wa Simba ni Manula, Kakolanya na Ali Salim. Manula amesema jijini Dar es...
michezo
['Mkufunzi wa Man United Ole Gunnar Solskjaer anahofia kwamba hatma ya kazi yake itakuwa haijulikani iwapo timu yake itashindwa kwa mabao mengi ugenini Liverpool.(Mail)', 'Baadhi ya wachezaji wamepoteza matumaini na raia huyo wa Norway anaamini baadhi yao wamekataa kumsikiliza. (Sun)', 'Solskjaer anahitaji kitita cha £...
michezo
Akijibu maswali ya gazeti hili kuhusu faida za gesi asilia katika uchumi wa taifa, Kisamo alisema kuwa matumizi yake yataendelea kuleta unafuu katika uchumi kulingana na jinsi matumizi ya gesi hiyo yatakavyoongezeka nchini siku hadi siku.“Gharama za kununua gesi asilia si za juu kama ilivyo za kununulia mafuta mazito,...
uchumi
HADI kufi kia juzi Serikali imefanikiwa kulipa jumla ya wakulima 82,835 katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma. Jumla ya fedha iliyolipwa kwa wakulima hao, ambao tayari wamefanyiwa uhakiki ni Sh bilioni 83.Walikuwa wamelipwa fedha hizo hadi juzi, ambapo katika mkoa wa Mtwara, wakulima 50,835 wamelipwa, mkoa wa Lindi ...
kitaifa
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amezindua Mkakati wa Nne wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi 2018/19 hadi 2022/23 wenye lengo la kuimarisha Kampeni ya Kupambana na Ukimwi na kufikia ‘90 tatu’ ifikapo 2023.Akizungumza wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Ukimwi jijini Dodoma jana, alisema mkakati huo umezingatia matokeo ya mapiti...
kitaifa
TIMU za vijana waliochini ya umri wa miaka 17 za Ethiopia na Uganda leo zinatarajiwa kucheza fainali wa mashindano ya Cecafa ya kutafuta kufuzu Afcon 2019 utakaochezwa saa 11:00 jioni Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Ethiopia imefuzu fainali baada ya kuifunga Rwanda kwa penalti 4-2 baada ya kumaliza dakika 90 kwa sare y...
michezo
WATAALAMU wameshauri wanaume nchini waache kula vyakula vilivyokaangwa zikiwemo chipsi, baga, unywaji wa pombe, uvutaji sigara.Wameshauriwa wale zaidi vyakula aina ya njugu kama vile karanga, korosho, mbegu za maboga na jamii ya aina hiyo ili kuimarisha mbegu zao za uzazi.Wamesema, wanaume pia wanapaswa kula vyakula v...
kitaifa
Meneja Mkuu wa Kodi wa kampuni hiyo, JosephThogo alisema kushindwa kwa nchi hizo kuwa na vifaa vya kutosha vya kuhifadhia mafuta kunamaanisha kwamba zitashindwa kujikusanyia mafuta ya kutosha kwa bei nafuu kama zinavyofanya nchi nyingine duniani.Alisema kwa miezi michache iliyopita, bei ya mafuta duniani imeshuka kwa ...
uchumi
RWANDA imeshika nafasi ya pili kwa umaarufu Afrika katika kuandaa mikutano na makongamano ya kimataifa. Shirika la Kimataifa la Uandaaji Mikutano (ICCA) imeeleza kuwa Afrika Kusini imeshika nafasi ya kwanza.Mwaka jana Kigali ilishika nafasi ya tatu ikitanguliwa na Cape Town na Morocco. Taarifa iliyotolewa na ICCA, ina...
kitaifa
Kwa mujibu wa ratiba hiyo iliyotolewa juzi, Rwanda itacheza na Kenya mchezo wa raundi ya kwanza ya kufuzu huku mchezo wa kwanza ukipigwa Nairobi kati ya Machi 30 na Aprili mosi, na marudiano yatafanyika Aprili 20-22.Mshindi wa jumla wa mechi hizo mbili kati ya Rwanda na Kenya atakutana na bingwa mtetezi Zambia katika ...
michezo
MBUNGE wa Viti Maalumu, Mariamu Ditopile amewataka wakazi wa kijiji cha Godegode na Pwaga, wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma, kuwa wavumilivu wakati serikali inaendelea kukabiliana na tatizo la ukosefu wa maji kama ilivyoahidi.Kauli hiyo aliitoa baada ya kusikiliza kilio cha wakazi wa eneo hilo wakati akiwa katika ziara ...
kitaifa
NDEGE nyingine mbili kubwa zilizonunuliwa na serikali ili kuendelea kuboresha Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) zitawasili nchini Desemba, mwaka huu.Hayo yalibainishwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe wakati akifungua mjadala wa wazi wa siku mbili, ulioshirikisha wadau wa sekta ya anga jana,...
kitaifa
WADAU wa bandari kutoka Afrika na baadhi ya nchi za Bara la Ulaya wamekutana jijini Dar es Salaam kujadiliana kuhusu masuala yanayohusu bandari zikiwemo fursa za kiuchumi za uendelezaji wa bandari hizo.Mkutano huo wa tatu ujulikanao kama ‘Utanuzi wa Bandari Afrika’ pamoja na kujadili masuala yanayohusu upanuzi wa band...
uchumi
KOCHA wa zamani wa timu ya Soka ya Taifa,Taifa Stars Dk. Mshindo Msolla amemshauri kocha wa timu hiyo Emmanuel Amunike kufanya kazi kwa uhuru hususani kwenye uteuzi wa kikosi kinachoenda kuiwakilisha nchi kwenye michuano mikubwa.Msolla ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku chache zimepita baada ya Amunike kuteua kikosi cha ...
kitaifa
HOSPITALI ya Rufaa ya taifa ya Mirembe haikujengwa mkoani Dodoma kutokana na mkoa huo kuwa na wagonjwa wengi wa akili (vichaa) bali kuwepo kwa gereza la Isanga ambalo wanafungwa wahalifu wakubwa na wauaji wanaotakiwa kupimwa akili zao.Naibu Waziri wa Afya, Maendelelo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndug...
kitaifa
KAMATI ya Kudumu ya Maendeleo ya Wanawake, Habari na Utalii ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, imeipongeza kampuni ya magazeti ya serikali (TSN) kwa kuja na mbinu mpya za kujiendesha kibiashara.Kwa sasa kampuni hiyo inayozalisha magazeti ya HabariLEO, Daily News na SpotiLeo, imekuja na miradi mipya ikiwamo kuwa na shi...
uchumi
WASOMI wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) wakishirikiana na Umoja wa maveterani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamemuomba Rais John Magufuli kuruhusu lugha ya Kiswahili kutumika kufundishia elimu ya sekondari nchini.Wasomi hao wakiongozwa na Profesa Aldin Mutembei walikutana jana Dar es Salaam na uongozi wa umoja huo ul...
kitaifa
MITI 4,170,076 sawa na asilimia 73.4 kati ya mti 5,356,887 iliyopandwa kati ya mwaka 2017 na 2018 mkoani Lindi imepona na kuendelea kukua.Taarifa hiyo imetolewa na Ofi sa Maliasili na Mazingira wa Mkoa wa Lindi, Zawadi Jilala wakati wa maadhimisho ya siku ya upandaji miti kimkoa iliyofanyika wilayani Kilwa. Jilala ali...
kitaifa
MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba jana walilipa kisasi baada ya kuifunga Mashujaa ya Kigoma kwa bao 1-0 katika mchezo wa kirafi ki uliofanyika kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.Ushindi huo wa Simba ni sawa na kulipa kisasi baada ya vigogo hao wa soka nchini kufungwa 3-2 na kutolewa katika michuano ya Kom...
michezo
WIZARA ya Fedha na Mipango imetoa orodha ya kwanza ya wadaiwa sugu wafanyabiashara 15 walionufaika na Mpango wa Kusaidia Uingizwaji wa Bidhaa nchini (CIS) na FACF, wafanyabiashara Mohamed Dewji na Yusuf Manji ni kati ya wadaiwa hao.Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na wizara hiyo, imewataka ...
kitaifa
UBALOZI wa Tanzania nchini Ujerumani umesikitishwa na kitendo cha Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kutoa tuhuma nzito dhidi ya Rais John Magufuli na serikali kuhusu ufi nyu wa demokrasia nchini.Kwa mujibu wa ubalozi huo, kitendo anachoendelea kukifanya mbunge huyo cha ziara za vyombo vya habari katika nchi mba...
kitaifa
SERIKALI imesema itaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuhakikisha kuwa inaongeza uwiano wa jinsia baina ya wanaume na wanawake katika vyombo vya uamuzi ili kufi kia 50 kwa 50.Ili kufikia hilo, imetaja mikakati iliyoanza kuchukuliwa ili kuzijengea uwezo jinsia zote, ikiwemo ya kufuta kodi za pedi za kike ili kuwezes...
michezo
SERIKALI imeeleza mpango wake wa kusukuma mbele viwanda na kufanya biashara nchini kwa kuhakikisha inatekeleza mfumo rafi ki wa uwekezaji na ufanyaji biashara nchini. Imesema katika kuendeleza ujenzi wa uchumi wa viwanda serikali itaendelea kuweka vivutio na kufanya maboresho katika maeneo kadha yanayoleta vikwazo ili...
kitaifa
SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeanza kuhakiki malipo kwa ajiri ya wanachama wake, waliokuwa wakifanya kazi zisizo za weledi kwenye sekta mbalimbali kabla ya kuachishwa kazi.Hatua hiyo imekuja baada ya agizo la Rais John Magufuli alilolitoa, alipokutana na viongozi wa vyama vya wafanyakazi Desemba 28 mw...
kitaifa
MBUNGE wa Chemba, Juma Nkamia (CCM) amesema ni aibu Tanzania kuchukua makocha kutoka nje huku kukiwa na wazawa wenye uwezo mkubwa.Akichangia taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kwa mwaka 2018-2019, Nkamia alisema ni aibu kwa kocha wa mpira wa miguu kutoka Bur...
michezo
Hatua hiyo inatoa fursa kwa huduma hii mpya ya malipo ya kabla ya kutumia kadi ya kielektroniki la daraja la juu inayotumia mfumo wa kibenki, kufanyika katika wigo mpana ndani na nje ya Tanzania.Makubaliano hayo sasa, yatamwezesha mtumiaji wa huduma za B-PESA kuweza kufanya mwamala nje ya Tanzania katika mashine za ku...
uchumi
WATAZAMAJI wanatakiwa kutoa kiasi cha Sh 5,000 ili kuiona Simba ikicheza dhidi ya Mbabane Swallows ya eSwatini katika mchezo wa awali wa kuwania kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa wa Afrika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo.Mchezo huo wa kwanza wa raundi ya awali, umepangwa kuanza majira ya saa 10:00. Ofisa...
kitaifa
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imekuwa inatumia wastani wa Sh bilioni tatu kila mwaka kusafi risha wagonjwa nje ya nchi kwa ajili ya kupata huduma za matibabu, tayari imeanza kuchukua hatua za kukabili changamoto hiyo.Hatua iliyochukuliwa ni ile ya kuingiwa kwa makubaliano baina ya Hospitali ya Taifa ya Muhim...
kitaifa
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Gor Mahia, Meddie Kagere ameibuka na kusema kuwa nusura atue kwa wapinzani wa timu hiyo ya Kenya, AFC Leopards kabla ya kusajili Gor.Akizungumza katika mahojiano na Sunday Nation, Kagere mwenye umri wa miaka 32 aliendelea kuichezea K’Ogalo kwa sababu tu viongozi hawakutokea kuzungumza naye ku...
michezo
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umekanusha taarifa zisizo rasmi kuhusu kuwepo kwa viwango vipya vya michango ya uanachama katika kupatiwa huduma za afya.Hata hivyo ilibainishwa jana kuwa upo mchakato wa kuunda vifurushi tofauti vya uchangiaji kwa makundi tofauti ya uanachama ili kuwezesha watu kujiunga kulingana...
kitaifa
KOCHA wa Tanzania Prisons, Mohammed ‘Adolf’ Rishard, amesema hawatakubali rekodi yao ya kutokufungwa kwenye Ligi Kuu ivunjwe na Yanga kwenye mchezo utakaochezwa kesho katika Uwanja wa Sokoine, mkoani Mbeya.Tanzania Prisons ambayo imecheza michezo 13 na kushika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 23 n...
michezo
UONGOZI wa JKT Oljoro ya jijini Arusha ambao ndio wamiliki halali wa timu ya Arusha United wameiuza timu hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti. Hatua hiyo imekuja wiki chache baada ya Mkuu wa Mkoa Arusha, Mrisho Gambo kudaiwa kushindwa kuiendesha timu hiyo ikiwa inashiriki Ligi Daraja la Kwanza.Meneja wa ...
kitaifa
UPELELEZI katika kesi ya kuchapisha video ya ngono kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram inayomkabili, Msanii wa Filamu nchini, Wema Sepetu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, bado haujakamilika.Wakili wa Serikali, Jenipher Masue alidai jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Maira Kasonde kuwa kesi hiyo imekuja kwa aji...
kitaifa
MAREKEBISHO ya Sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza Sura ya 230 yanayojumuisha mapendekezo ya kuzirasimisha kumbi au vibanda vinavyotumika kuoneshea video na hivyo kuratibiwa na sheria hiyo ya filamu, yamepitishwa rasmi na Bunge.Aidha, marekebisho hayo yameweka masharti kwa mtu au kampuni ya kigeni inayotaka kutumia...
michezo
Akizungumza jana Dar es Salaam wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa, Uchuuzaji na Mikakati wa Benki hiyo, Musa Kitoi alisema mashine hizo za kisasa za i-ATMs zimetengenezwa kwa teknolojia ya juu na zina sifa ya kipekee.Alisema huduma mbalimbali kama kuweka na kutoa fedha taslimu na hundi...
uchumi
TIMU ya Yanga jana ilipindua meza kibabe baada ya kuwa nyuma kwa mabao 3-1 na kulazimisha sare ya 3-3 na kunusurika na kichapo katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.Huu ni mchezo wa pili kwa Yanga kushuka dimbani baada ya kucheza mchezo wa kwanza, ambao walipoteza dhidi ya...
michezo